Monday, December 9, 2013

WELCOME ALL VIEWERS TO OUR BLOG SEPSSA

SEPSSA (SEKOMU POLITICAL SCIENCE STUDENTS ASSOCIATION)



Tunawakaribisha wasomaji wote katika blog yetu ya Kisiasa na Kielimu kwa ajili ya mababiliko chanya ya nchi yetu Tanzania na bara la Africa kwa ujumla.
SISI NI NANI?
Jumuiya  hii ni ya wanachuo wanaosoma na waliowahi kusoma Sayansi ya Siasa na Utawala katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa. Jumuiya hii inazingatia misingi ya UWAZI, HAKI, UDUGU na AMANI.
Dira
Dira letu kuu ni kulinda utu, amani na hadhi ya taaluma ya Sayansi ya siasa na utawala pamoja na kusaidia kwa huruma jamii ya Tanzania ili kuboresha maisha katika hali ya kujenga ufahamu wa kielimu, kuleta mabadiliko yanayoleta tija kwa wakati uliopo na ujao na matumizi sahii ya rasilimali watu na vitu katika nchi hii.
Jina la jumuiya yetu ni Sekomu Political Science Students Association (SEPSSA). Hii ni jumuiya ya Wanachuo wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa.
Mlezi na mshauri wa shughuli zote za jumuiya hii ni Mkuu wa idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa.
Malengo ya SEPSSA ni:
1.      Kutetea, kuchambua na kutoa mapendekezo yatakayoboresha mfumo wa siasa katika jamii ya Tanzania,
2.      Kulinda na kuboresha maisha ya watanzania kwa kuhimiza matumizi sahihi ya rasilimali za nchi
3.      Kuwa kiungo cha mahusiano na taasisi za ndani na nje ya chuo katika mambo ya siasa na utawala
4.      Kuandaa na kushiriki katika mijadala na makongamano ya kitaifa na kimataifa
5.      Kutoa elimu ya uraia katika masuala mbalimbali kwa ustawi wa jamii ya kitanzania
Moto:
SEPSSA for Change in Education, Resource and Service

No comments:

Post a Comment