SEPSSA (SEKOMU POLITICAL SCIENCE STUDENTS ASSOCIATION)
Tunawakaribisha
wasomaji wote katika blog yetu ya Kisiasa na Kielimu kwa ajili ya mababiliko
chanya ya nchi yetu Tanzania na bara la Africa kwa ujumla.
SISI NI NANI?
Jumuiya hii ni ya wanachuo wanaosoma na waliowahi
kusoma Sayansi ya Siasa na Utawala katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa. Jumuiya hii inazingatia misingi
ya UWAZI, HAKI, UDUGU na AMANI.
Dira
Dira letu kuu ni
kulinda utu, amani na hadhi ya taaluma ya Sayansi ya siasa na utawala pamoja na
kusaidia kwa huruma jamii ya Tanzania ili kuboresha maisha katika hali ya
kujenga ufahamu wa kielimu, kuleta mabadiliko yanayoleta tija kwa wakati uliopo
na ujao na matumizi sahii ya rasilimali watu na vitu katika nchi hii.
Jina la jumuiya yetu ni
Sekomu Political Science Students Association (SEPSSA). Hii ni jumuiya ya
Wanachuo wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa.
Mlezi na mshauri wa
shughuli zote za jumuiya hii ni Mkuu wa idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala
katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa.
Malengo ya SEPSSA ni:
1.
Kutetea, kuchambua na kutoa mapendekezo
yatakayoboresha mfumo wa siasa katika jamii ya Tanzania,
2.
Kulinda na kuboresha maisha ya
watanzania kwa kuhimiza matumizi sahihi ya rasilimali za nchi
3.
Kuwa kiungo cha mahusiano na taasisi za
ndani na nje ya chuo katika mambo ya siasa na utawala
4.
Kuandaa na kushiriki katika mijadala na
makongamano ya kitaifa na kimataifa
5.
Kutoa elimu ya uraia katika masuala
mbalimbali kwa ustawi wa jamii ya kitanzania
Moto:
SEPSSA for Change in Education,
Resource and Service
No comments:
Post a Comment